Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema Rais Edgar Lungu wa Zambia anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya siku tatu nchini kuanzia Novemba 27 kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Mahiga amesema wakati wa ziara hiyo, Rais Lungu atasaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Zambia na Tanzania.

Miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na ushirikiano wa masuala ya anga, ulinzi na usalama, ushirikiano katika masuala ya uhamiaji, na kuweka utaratibu wa kubadilishana wafungwa.

Akiwa nchini Rais Lungu pia atatembelea Bandari ya Dar es Salaam, reli ya Tazara, na bomba la mafuta la Tazama.

Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya Afrika Balozi Samweli Shelukindo amesema utekelezaji wa mikataba hiyo utaleta maendeleo baina ya nchi hizi mbili.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *