Rais wa Zambia, Edgar Lungu amewatahadharisha majaji nchini humo kwamba kutazuka vurugu nchini humo iwapo watathubutu kumzuia kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2021.
Amesema hawafai “kuwaiga” majaji wa Kenya ambao walitumbukiza nchi hiyo kwenye mzozo baada ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti ambapo Rais Kenyatta alikuwa ametangazwa kuwa mshindi.
Kumezuka mjadala kuhusu iwapo Lungu anafaa kuwania au la, huku wakosoaji wake wakisema kwamba anahudumu muhula wa pili na hivyo hawezi kuwania tena.
Wanasema kipindi ambacho alihudumu baada ya kifo cha Rais Michael Sata mwaka 2014 kinafaa kuhesabiwa kama muhula wa kwanza.
Wafuasi wa Lungu wanasisitiza kwamba alimaliza tu muhula wa mtangulizi wake na kwamba muhula wake wa wkanza ulianza aliposhinda uchaguzi wa 2016, ambao ulikumbwa na utata.
Watu wanasema kwamba mahakama za Zambia zinafaa kufuata mfano wa mahakama za Kenya.
Watu wanasema mahakama za Zambia zinafaa kwua na ujasiri na kufanya maamuzi ambayo yanazingatia maslahi ya raia, lakini hebu tazameni yanayotokea Kenya sasa.