Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye amehukumiwa kwenda jela miaka 24 kwa makosa ya rushwa.

Geun amekutwa na makosa 18 ikiwemo kutumia vibaya madaraka yake na kupokea rushwa hivyo mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miaka 24 gerezani.

Hakimu huyo aliongeza kuwa hukumu kali ilihitajika ili kutuma ujumbe wa wazi kwa viongozi wa baadaye wa nchi hiyo.

Hata hivyo waendesha mashitaka walimwomba Hakimu kumhukumu Geun kifungo cha miaka 30 jela. Pia Rais huyo wa zamani wa Korea Kusini atatakiwa kulipa faini ya dola milioni 17 mbazo ni zaidi ya shilingi bilioni 38 za Kitanzania.

Kesi ya Geun ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanaza January 3 mwaka jana japo kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria mahakamani hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *