Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, atakabiliwa na mashtaka ya kuzuia utekelezaji wa haki.

Stakabadhi kutoka mahakama moja ya Brasilia zinaonyesha kuwa Lula ameshtakiwa pamoja na watu wengine sita.

Amekuwa akichunguzwa chini ya mpango ujulikanao kama Operation Car Wash, unaochunguza ufisadi unaolenga shirika la mafuta la Serikali la Petrobus.

Mnamo mwezi Mei, mwanasheria mkuu wa Brazil, Rodrigo Janot, alimlaani Lula kwa kushiriki katika kashfa hiyo, ambayo iligharimu shirika hilo dola bilioni mbili.

Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *