Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amewataka viongozi wa mataifa ya kiislamu duniani kuutambua mji wa Jerusalem kama mjii mkuu wa Palestina.
Amesema hayo leo wakati akihutubia mkutano wa viongozi wa kiislamu dunia ulioitishwa ghafla kwa ajili ya kujadili kauli ya rais wa Marekani, Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Rais Erdogan amesema kuwa kitendo cha rais Trump kuutambua mjii wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel ni kitendo cha kijinga na akiungiw mkono na mataifa mengi.
Pia rais Erdogan ameishtumu nchi ya Israel kwa kuliita taifa la kigaidi ambalo linataka kuchukua mji wa Palestina.
Kwa upande wa kiongozi wa Palestinian, Mahmoud Abbas amesema kuwa Marekani haiwezi kuwa miongoni mwa nchi suluhishi kwasababu wameegemea sana upande wa Israel.