Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte amekiri kwamba alimuua mtu kwa kumchoma kisu akiwa kijana.
Duterte amewahi kusema awali kwamba aliwaua washukiwa wa uhalifu alipokuwa meya wa mji wa Davao.
Kiongozi huyo wa Ufilipino anahudhuria mkutano huo wa Apec pamoja na viongozi wengine akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump.
Duterte anatarajiwa kushauriana moja kwa moja na Rais wa Marekani Donald Trump siku chache zijazo – mkutano wa kwanza kati ya wawili hao.
Rais huyo wa Ufilipino ameongoza kampeni yenye utata ya kukabiliana na wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya.
Wakosoaji wake wanasema kampeni hiyo imehusisha ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu.
Duterte amewahamasisha watu kuua washukiwa wanaohusika na dawa za kulevya bila kuwafikisha kwa polisi na alisema anaweza kufurahia sana iwapo angeweza kuwaua waraibu milioni tatu wa mihadarati nchini humo.
Akihutubia raia wa Ufilipino mjini Da Nang, amesema alimuua mtu wakati wa ukali wake miaka yake ya ujana na kwamba kulikuwa na vita vingi pamoja na “kuingia na kutoka jela” mara kwa mara.