Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema amemshamwishi Rais wa Marekani Donald Trump, asiviondoe vikosi vya askari wa Marekani vilivyoko nchini Syria.

Mapema mwezi huu, Rais Trump alisema kwamba ataviondoa vikosi vya askari wake vipatavyo elfu mbili ambavyo vilitumwa nchini Syria hivi karibuni.

Ingawa Rais wa Macron amewaambia waandishi habari nchini kwamba amezungumza na rais Trump kabla ya shambulizi la anga lililotekelezwa mwisho mwa juma lililopita na kumtaka ashiriki kutafuta suluhu ya mgogoro huo kwa muda mrefu zaidi.

Akitolea ufafanuzi juu ya shambulio hilo la anga lililotekelezwa kwa pamoja baina ya Marekani, Ufaransa na Uingereza kwamba lilikuwa la halali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *