Rais wa Sudan, Omar el Bashir amempongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump huku akisema kuwa itakuwa rahisi kushirikiana naye.
Rais alisema kuwa Trump anaangazia maslahi ya raia wa Marekani, ikilinganishwa na wale wanaozungumzia kuhusu demokrasia ,haki za kibinaadamu na uwazi.
Pia aliongezea kwa kusema kuwa “Tunaweza kushirikina na watu wenye sura mbili lakini huyu hapa mtu mwenye uwazi wa anajua anacholenga”.
Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya ICC kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika eneo la Drafur amekana mashtaka hayo.
Rais huyo alichukua madaraka mwaka 1989 kupitia mapinduzi na ameshutumiwa kwa kuwa na uongozi wa kiimla tangu wakati huo.