Rais wa Sudan Omar al-Bashir amealikwa kwenye mkutano nchini Saudi Arabia ambao utahudhuriwa na rais wa Marekani Donald Trump.
Al-Bashir anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kivita (ICC) kwa mashtaka ya uhalifu ya kivita aliyoshiriki nchini mwake.
Ila bado rais huyo hajakubali mwaliko huo na haijulikani kama Bashir akakubali mualiko huo kutoka Saudia.
Kwa upande wake Trump anatarajiwa kuwasili nchini Saudi Arabia siku ya Jumamosi wakati anapoanza ziara yake ya kwanza ya kigeni nchini humo.
Rais huyo wa Sudan anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, kufuatia uhalifu uliotokea jimbo la Dafur nchini Sudan.
Marekani si mwanachama wa mahakama ya ICC lakini imeunga mkono kazi zake kutoka mahakama hiyo yenye makoa makuu The Heague nchini Uholanzi