Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amekutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kwenye eneo la mstari wa kijeshi uliowekwa kuyagawa mataifa hayo mawili tangu vita vya Korea mwaka 1953.

Msemaji wa Rais Korea Kusini, Yoon Young-chan amesema kuwa kikao hicho cha viongozi hao wawili kimedumu kwa dakika 100.

Yoon ameongeza kuwa mkutano huo ambao unaajenda kuu tatu utaangazia masuala ya nchi hizo mbili ikiwemo silaha za nyuklia na kuboresha mahusiano, na kutafuta makazi ya amani rasmi.

Mwishoni mwa mwezi March mwaka huu Kim Jong-un alifanya ziara nchini China na kukutana na Rais Xi Jinping mjini Beijing. Hiyo ilikuwa ziara yake ya kwanza kufanya nje ya taifa lake la Korea Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *