Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow leo anatarajiwa kidhinishwa rasmi kuwa kiongozi wa taifa hilo kufuatia kuondoka kwa Yahya Jameh, mwezi mmoja uliopita.

Maelfu ya watu, kukiwemo viongozi kadhaa wa Afrika wanatarajiwa kuhudhuria hafula hiyo katika mji mkuu wa Banjul.

Rais Barrow aliapishwa kuwa rais mwezi uliopita katika ubalozi wa Gambia katika taifa jirani la Senegal kabla ya mtangulizi wake kukubali kung’atuka mamlakani.

Bwana Jammeh alikuwa amekataa kukubali kushindwa katika Uchaguzi wa Disemba na aliondoka nchini tu baada ya kushinikizwa kufanya hivyo na viongozi wa mataifa ya Magharibi mwa Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *