Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein leo amewaongoza maelfu ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Sherehe za maadhimisho yamefikia kilele hii leo katika uwanja wa amani visiwani humo huk viongozi mbalimbali wa serikali za pande zote mbili, mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wamehudhuria sherehe hizo.

 

Rais Shein amekagua gwaride maalum lilioandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo ya mapinduzi matukufu katika visiwa hivyo vya Zanzibar.

 

Kwa upande wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, yeye ataongoza wananchi wa Tanzania Bara katika maadhimisho hayo akiwa mjini Shinyanga kwa mkutano mkubwa wa hadhara unaofanyika katika uwanja wa Kambarage.

 

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12 mwaka 1964 yakiongozwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume kwa kumuondoa aliyekuwa mtawala wa visiwa hivyo Sultan Sayyid Said.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *