Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa nch hiyo.
Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo ya waziri wa fedha.
Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
Palipotokea anguko la thamani ya randi alilazimika kumfukuza Rooyen na kumchagua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi siku za mbeleni.
Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.
Aliyekuwa mke wake Zuma, Nkosazana Dlamini-Zuma, ameteuliwa kuwa waziri wa ofisi wa rais.
Bw Ramaphosa, ambaye ni mfanya biashara wa umri wa miaka 65, katika hotuba yake ya taifa awali mwezi huu, aliahidi kupambana na rushwa na kuboresha uchumi wa nchi hio.
Aliingia madarkani baada ya mtangulizi wake kuondoka katika hali tete, akikataa shinikizo kubwa ya yeye kujiuzulu.
Utawala wa miaka tisa ya Bw Zuma ulikumbwa na misukosuko ya shutuma za ufisadi wakati nchi ilikuwa ikipambana na madeni ya ndani pamoja na viwango vya juu vya ukosaji ajira.