Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Mgufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ itakayozinduliwa Ijumaa, Disemba 8, mwaka huu.

Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ itaratibiwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Msanii wa Muziki wa Asili Tanzania, Mrisho Mpoto kupitia Kikundi chake na wadau wa sanaa za ubunifu ndiyo watasherehesha kwa burudani katika usiku huo wa Kitendawili.

Kwa upande wake Mrisho Mpoto amesema, kampeni hiyo ina lengo la kurejesha hali ya Uzalendo na Utaifa katika kutatua changamoto zilizojitokeza na zitakazojitokeza ndani ya taifa letu.

 Mambo yatakayozungumza kwenye usiku huo ni kudhibiti na kukomesha mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa umma, kuongezeka kwa tuhuma za rushwa, kuibuka kwa ufisadi, ubadhilifu wa mali za umma na kuongeza hali ya kufanya kazi na Uzalendo.

Mpoto aliongeza kuwa, lengo kuu la maadhimisho hayo kuambatana na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa kuanzia mwaka 2018 ni kutumia jukwaa hilo kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kujenga na kuendeleza Utaifa.

Baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo kufanyika mjini Dodoma, pia itafanyika kwenye mikoa yote nchini na itasimamiwa na Kamati za Utamaduni za mkoa na wilaya.

 Usiku wa Kitendawili ulianzishwa baada ya Mpoto kuachia Wimbo wa ‘Kitendawili’ na baadaye kufikiria kuanzisha usiku wa wimbo huo na kuanzisha mjadala kuhusu uzalendo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *