Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli jana amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Kahitwa Bishaija na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa TANESCO Bw. Sadock Mugendi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuanza kulipa deni inalodaiwa na TANESCO.

Prof. Muhongo amesema tayari SMZ imeanza kulipa kiasi cha Shilingi Bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.

Pia Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa sugu wote wa TANESCO kulipa madeni yao katika kipindi cha siku 5 zilizobaki kwa kuwa wasipolipa watakatiwa umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *