Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua stendi ya kisasa ya mabasi wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Stendi hiyo ya kisasa ina uwezo wa kupaki magari mengi yenye uwezo wa kusafiri ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kusafirisha abiri watakafika kituo hapo kwa ajili ya kupata huduma ya usafiri.

Uzinduzi wa stendi hiyo umehudhiriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali akiwemo waziri wa Afya, Ummy Mwalim, Naibu waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo, Wziri wa Muungano, January Makamba pamoja na wabunge wa Mkoa wa Tanga.

Muonekano wa stendi ya Korogwe iliyozinduliwa leo na Rais Magufuli.
Muonekano wa stendi ya Korogwe iliyozinduliwa leo na Rais Magufuli.

Katika uzinduzi huo, Rais Magufuli amewataka wananchi wa Korogwe na Tanga kwa ujumla kuilinda stend hiyo pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo baada ya kukamilika kwa stendi hiyo ya kisasa.

Rais Magufuli leo amehitimisha ziara yake ya siku tano mkoani Tanga ambapo ameweka jiwe la msingi la bomba la mafuta kutoka Tanga hadi nchini Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *