Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amezindua barabara ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga iliyogharimu sh. bilioni 190.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo, Rais Magufuli amesema kwamba Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umasikini na wananchi wanafanya ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.
Uzinduzi huo pia umehudhuriwa na waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Waziri Mbarawa ametoa tamko hilo leo wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu ambao wamehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 154.
Kwa upande wake Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa amesema wanaunga mkono msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuendelea na masomo na wameanzisha shule ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli yake.