Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi na waumini wa Kanisa la Anglikana na madhehebu mengine, kwa kuendelea kuliombea Taifa na kudumisha amani ma utulivu.

Amesema hayo jana alipoungana na waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, Dar es Salaam, kusali ibada ya Jumapili ya kuadhimisha Siku ya Bwana ya 19 baada ya Pentekoste.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa, Rais aliongozana na mkewe, Mama Janeth.

Amesema Rais wakati akizungumza na waumini wa kanisa hilo baada ya kumalizika kwa Ibada, aliwashukuru viongozi na waumini wote nchini kwa kuendelea kuliombea Taifa.

Rais Magufuli alisisitiza kuwa viongozi wa dini, wanafanya kazi kubwa na muhimu katika Taifa na kwamba watanzania wote bila kujali dini zao, itikadi za kisiasa, makundi na kada zao, wana wajibu wa kuungana na viongozi hao ili nia hiyo njema iendelee kufanikiwa.

Kwa upande wake, Padre Jackson Sostenes aliyeongoza ibada hiyo, alimshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na waumini wa kanisa hilo katika ibada ya Jumapili na aliahidi kuwa viongozi na waumini wa kanisa hilo, wataendelea kumuombea na kuliombea Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *