Baada ya wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kusimamishwa kazi kutokana na kutangaza habari ya uongo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewasamehe wafanyakazi hao.

Wafanyakazi hao walirusha hewani taarifa ya uongo iliyosambazwa na mtandao wa Fox Channel.com kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amesifu utendaji kazi wa Rais Magufuli.

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba, ilieleza kuwa makosa hayo yalileta usumbufu kwa umma na yasingefanyika endapo taratibu zote za kitaalamu zingefuatwa kuthibitisha ukweli wa taarifa yenyewe.

Watangazaji waliotangaziwa msahama huo ni Rais Dkt Magufu ni pamoja na Gabriel Zackaria, Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.

Rais Dkt Magufuli alitoa msamaha huo alipofanya ziara katika kituo hicho jana ili kuangalia utendaji kazi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi kuweza kutambua changamoto zinazowakabili.

Wafanyakazi hao walisamishwa kazi mwezi Machi kwa kuhusika katika makosa ya kiweledi na kiuhariri yaliyosababisha kutangazwa kwa taarifa ambayo haikuwa sahihi Machi 03, 2017.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *