Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amewapongeza Mabalozi sita waliochaguliwa na nchi zao kuja kuziwakilisha nchini Tanzania huku akiwaahidi kuwapa ushirikiano utakaowezesha kukuza pande zote mbili.
Rais Magufuli akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga (aliyevalia suti nyeusi) kwa Balozi wa Ethipia hapa nchini Dina Mufti Saidi
Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akipokea hati za utambulisho za Mabalozi hao ambao ni Mhe. Konstantinos Moatsos Balozi wa Ugiriki hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Fafre Camara Balozi wa Mali hapa nchini mwenye makazi yake Addis Ababa nchini Ethiopia na Mhe. Dina Mufti Sid Balozi wa Ethiopia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya.
Wengine ni Mhe. Elizabeth Taylor Balozi wa Colombia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Martin Gomez Bustillo Balozi wa Argentina hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya na Mhe. Uriel Norman R. Garibay Balozi wa Ufilipino mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya.
Pamoja na hayo Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kufikisha salamu zake kwa viongozi wa nchi zao na kuwakaribisha kutembelea Tanzania.