Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameahidi nyongeza za mishahara na kuwapandisha daraja wafanyakazi wanaostahili.

Rais Magufuli amesema kuwa baada ya serikali kukamilisha zoezi la kuwasafisha watumishi hewa, na kutangaza kutoa ajira mpya 52,000 katika mwaka huu.

Rais Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo jana Mkoani Kilimanjaro katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika katika uwanja wa Ushirika.

Amesema kuwa wafanyakazi hao walikuwa wakiingiza serikali hasara ya shilingi bilioni 19.84 kwa mwezi zaidi ya shilingi bilioni 230 kwa mwaka, jambo ambalo iwapo angeongeza mishahara watumishi hao hewa nao wangenufaika.

Rais Magufuli amesema katika bajeti ya mwaka ujao Serikali itaongeza nyongeza za mshahara ya wafanyakazi wa umma ya kila mwaka, pamoja na kuwapandisha madaraja wafanyakazi, jambo ambalo lilikuwa limesimama kwa muda kupisha zoezi la kusafisha wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki.

Pia Rais Magufuli ameagiza mfanyakazi yoyote atakayehamishwa bila ya kupewa fedha zake za uhamisho asikubali kuhama, bila ya kupewa fedha hizo, na kuongeza kuwa kunawakati mwingine wafanyakazi wanahamishwa na maboss zao kwa kuonewa au kuonewa wivu tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *