Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya watu wanaopanga kuandamana akidai kuwa huu sio muda wa maandamano bali ni muda wa kujenga taifa.
Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akizundua tawi la benki ya CRDB wilani Chato mkoani Geita.
Rais Magufuli amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanapenda kuona Tanzania ikiwa na migogoro kila siku na wanafurahi kuona watu wanaandamana mabarabarani.
Kauli hiyo ya Rais Magufuli imekuja wakati kukiwa na taarifa zikizagaa mitandaoni kuwa kuna watu wanapanga maandamano yasiyo rasmi.
Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewataka Watanzania kufanya kazi na kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha mwanzo hadi tutakapofika kwenye nchi ya asali.