Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbarawa kupeleka bilioni 9 Mwanza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege.

Rais Magufuli ameagiza hilo leo akiwa jijini Mwanza wilaya ni Ilemela katika uzinduzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha ambapo ametaka fedha zaidi ya bilioni 9 zipelekwe Mwanza katika upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ili uwe uwanja wa kimataifa.

Rais alisema “Nimesikia kuwa mkandarasi anadai zaidi ya bilioni tisa, sasa Waziri naagiza mwambie huyo mkandarasi kuwa wiki hii atapata hizo fedha zote bilioni tisa kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, nataka uwanja huu uwe uwanja wa kimataifa akamilishe uwanja huu kabla sijamaliza muda wangu, kwani asipokamilisha ndani ya muda huo hapo atalala jela, nataka wafanyabishara wa samaki wasiende nchi zingine kwa ajili ya kusafarisha samakai zao’

Mbali na hilo Rais Magufuli amesema serikali yake imekusudia kujenga meli kubwa itakayobeba watu 1200, na tani za kutosha na magari katika ziwa Victoria.

Rais Magufuli yupo jijini Mwanza katika ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo ziara hiyo imelenga kuzindua daraja la Furahisha ambalo tayari limeshazinduliwa na baadaye atazindua kiwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *