Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa.
Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara.
Pamoja na hayo, Mzee Majuto aliendelea kwa kusema “sisi wazee tunafarijika sasa hivi, viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Hii ndio raha ya kupata viongozi wenye msimamo”.
Pia Mzee Majuto amesema kupata sio rahisi kupata Rais mwenye misimamo na asiyekuwa na masihara kama Dkt. John Magufuli.