Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli jana ametembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuwahakikishia wananchi kuwaatahamia Dodoma hivi karibuni.
Rais Magufuli ameongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Rais Magufuli amesema pamoja na majengo ya Ikulu Serikali itajenga miundombinu mingine zikiwemo reli na barabara za lami zitakazounganisha maeneo ya vijiji vinavyozunguka Ikulu na mji wa Serikali.
Pia Rais Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa wote watakaoguswa na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya Serikali na wanaostahili kulipwa fidia watalipwa.
Rais Magufuli amemaliza kwa kutoa wito kwa wananchi hao kutumia fedha za fidia watakazolipwa kujenga makazi bora na kujipanga kufanya shughuli zenye manufaa kwao.