Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Dkt. John Pombe Magufuli leo ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli anatarajiwa kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara katika mikutano hiyo.

Leo asubuhi ameweka jiwe la msingi la kiwanda cha vigae cha Tanzaniania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga mkoani na kuelekea Lindi.

Rais Magufuli kesho ataendelea na ziara yake katika mkoa wa Mtwara kwa kukagua miradi ya maendeleo mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *