Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na tajiri namba moja dunia, Bill Gates ikulu jijini Dar es Salaam.

Tajiri huyo namba moja duniani yupo nchini kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta ya kilimo, Afya pamoja na mifumo ya kielektroniki wa upatikanaji wa taarifa.

Katika mazungumzo hayo, Bill Gates amesema kuwa taasisi yake kwa kushirikiana na Tanzania itatoa shilingi milioni 777,084 za kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo nchini.

Rais Magufuli akifanya mazungumzo na tajiri namba moja duniani, Bill Gates Ikulu jijini Dar es Salaam leo
Rais Magufuli akifanya mazungumzo na tajiri namba moja duniani, Bill Gates Ikulu jijini Dar es Salaam leo

Pia Bill Gates amesema kuwa anafurahishwa na maendeleo ya uchumi wa Tanzania pamoja na uongozi na msimamo wa rais Magufuli kuhusu miradi hiyo ili ilete maendeleo nchini.

Kwa upande wake rais Magufuli amemshukuru Bill Gates kwa mchango wake mkubwa unaotolewa na taasisi yake katika miradi ya maendeleo hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *