Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatimiza miaka 41 tangu kuanzishwa kwake Februari 5 mwaka 1977.

Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho ametuma salamu kwa wanachama wa CCM katika siku hii muhimu kwao.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twittter Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote wa chama hicho.

“Nawapongeza viongozi, wanachama na wapenzi wote wa CCM kwa kutimiza miaka 41. Tunaposherehekea mafanikio yetu tuendelee kutunza Amani na umoja wetu, tuchape kazi kwa maslahi ya nchi yetu na Serikali inayoongozwa na CCM”.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa Februari 5, 1977 baada ya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara kuungana na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha TANU kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *