Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza bandarini hapoa jana.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli amegundua magari 50 ambayo mmiliki wake hajajulikana toka yalipowasili.
Magari hayo ambayo yameelezwa kuletwa mwezi wa 6 mwaka 2015 yakiwa na magari ya jeshi la polisi, mpaka leo hayajatolewa bandarini hapo na yakiaelezwa kuwa na siri kubwa ambayo Rais mwenyewe anaifahamu, huku mzigo wa lawama ukienda kwa Jeshi la Polisi.
Kufuatia tukio hilo Rais Magufuli ametoa siku saba kwa TAKUKURU, Polisi na Wizara ya Uchukuzi kumpatia taarifa kamili juu ya magari hayo, ambayo mpaka sasa mmiliki wake hajajulikana.