Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema, uteuzi wa Bw. Ndunguru umeanzia toka jana baada ya kuteuliwa.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Ndunguru alikuwa Kamishna wa Sera, katika Wizara ya Fedha na Mipango.
Bw. Adolf Ndunguru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.