Mahakama Kuu nchini Kenya imeamua kwamba mashtaka ya uhalifu au madai hayawezi kufunguliwa dhidi ya Rais juu ya utendaji wake wa kazi katika kipindi ambacho alikuwa madarakani.
Kutokana na msingi huo wa kisheria Jaji Chacha Mwita aliliondoa jina la Rais Uhuru Kenyatta kutoka kwenye kesi iliyofunguliwa na mwanaharakati Okiya Omtatah akipinga uamuzi wake wa kuteua makatibu wakuu na makatibu tawala.
Ingawa Jaji Mwita hakutoa sababu za kuliondoa jina la Rais Kenyatta kutoka kwenye kesi, kwa namna fulani ni kama alikubaliana na maoni ya Mwanasheria Mkuu kwamba Rais ana kinga ya kutoshtakiwa.
Mwanasheria mkuu kupitia mwanasheria mwandamizi Jennifer Gitiri, aliomba mashtaka hayo yafutwe na kuondolewa kwa jina la Rais Kenyatta katika suala linalojadiliwa kwamba ni kinyume cha katiba kuanzisha mashtaka yoyote dhidi ya Mkuu wa Serikali.
Gitiri alimwambia Jaji Chacha kuwa hakuna ulazima kwa Rais Kenyatta kuingizwa katika suala hili kwa kuwa AG ana uwezo wa kuiwakilisha serikali ya kitaifa katika madai yoyote.
aliongeza.
Bunge kupitia kwa mwanasheria Mbarak Awadh Ahmed alijihusisha na mjibu maombi mwanasheria mkuu kwamba amewasilisha maombi ya kutafuta kupinga mamlaka ya mahakama kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Omtatah.