Rais wa Rwanda Paul Kagame anaapishwa leo kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa tatu wa miaka 7.
Hii ni baada ya kushinda uchaguzi wiki mbili zilizopita kwa kupata asilimia 98 ya kura zote kwenye uchaguzi huo.
Sherehe za kula kiapo zinafanyika kwenye uwanja wa taifa Amahoro mjini Kigali na kuhudhuriwa na viongozi kutoka sehemu mbalimbali.
zaidi ya marais 20 kutoka mataifa ya Afrika wanahudhuria sherehe hizo zitakazofanyika nchini humo.
Miongoni mwao ni rais wa Sudan Omar Al Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.