Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila ameanza mazungumzo na Mashirika ya kiraia na wanasiasa wa upinzani kuhusu mustakabali wa siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kushindwa kufikia maamuzi, mazungunzo yaliyokuwa yakiongozwa na maaskofu wa kanisa katoliki.
Mpaka sasa chama tawala na upinzani wameshindwa kuafikiana kuhusu uteuzi wa waziri mkuu ,Mazungumzo haya mapya wanatarajia jibu la rais Joseph Kabila kwa maskofu wa kanisa katoliki ambao walijaribu kupatanisha wanasiasa wa upinzani na wa chama tawala kwa muda wa miezi mitatu lakini jitihada zao zilishindikana.
Hata hivyo kufuatana na msimamo wa kila upande , wakishindwa kuafikiana kuhusu kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya ambae alipaswa kutoka upande wa upinzani baada ya kushindwa maskofu waliomba rais Joseph Kabila kujaribu mwenyewe kutautua mgororo huu lakini hadi sasa vyama vikuu vya upinzani vimemsusia rais huyo na kukataa kufanya uchaguzi .
Mjadala huu mpya unaweza kuchukua muda wa siku tatu na hapo baadae rais Kabila atatoa hotuba ya mwisho bungeni juu ya mgororo huo wa kisisisa.
Kwa sasa maeneo mengi ya nchi hiyo yako kwenye hali ya wasiwasi, huku baadhi ya shughuli mbalimbali mjini Kinshasa kusimama kama vile kufungwa kwa baadhi ya maduka,shule na baadhi ya ofisi