Maelfu ya watu wamefanya maandamano leo katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, kupinga uongozi wa Rais Macky Sall.

Wanataka kuachiliwa kwa wapinzani wa kisiasa wa Rais hasa, Meya wa Dakar, Khalifa Sall aliyekamatwa.

Amekuwa kuzuizini kwa mwezi mmoja kwa madai kuwa alishiriki katika kulaghai serikali kiasi kikubwa cha pesa.

Anaonekana na wengi kama mshindani mkali katika uchaguzi wa Urais utakaofanywa mwaka 2019 akiwa mshindani wa chama cha Socialist Party.

Maandamano hayo yaliandaliwa na kundi linalojiita tumechoka lililoundwa miaka mitano iliyopita dhidi ya aliyekuwa Rais wa zamani, Abdoulaye Wade.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *