Rais wa Marekani, Donald Trump amelipongeza baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini.
Trump ameandika katika mtandao wake wa Twitter, kwamba hatua hiyo ni ishara wazi kwamba ulimwengu unataka amani na wala sio mauti.
Vikwazo hivyo vilivyowasilishwa na Marekani vinaungwa mkono na China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kusini.
Kufuatia vikwazo hivi vipya uagizaji mafuta wa Pyongyang utapunguzwa hadi asilimia tisaini, huku raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika mataifa ya kigeni wakitakiwa kurudi makwao.
Wizara ya mambo ya nje ya Uchina imesema vikwazo hivyo havitarajiwi kuwa na athari kubwa za kibinadamu.
Hata hivyo imetowa wito kwa pande zote kushauriana ili kujaribu kupunguza taharuki katika rasi ya Korea.