Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rachel amefunguka kuhusu sakata la kwenda nchi za Uarabuni na kukutwa na mabalaa ikiwemo kutumia madawa ya kulevya na kutelekezwa huko na mwanaume aliyekwenda naye.

Rachel amesema ni kweli alikwenda Uarabuni kwani ilikuwa ndoto yake tangu utotoni, na alipokwenda hukomilikuwa ni kutimiza ndoto zake na kuamua kubaki kwa muda kula raha.

Pia amesema kuwa “Kweli nilienda na nilienda na kazi zangu sio kwa ajili ya mapenzi, nakuhusu kubaki kule kule sikutamani, lakini ndoto zangu tangu niko shule ilikuwa kufika kwenye nchi za Uarabuni.

Pia amesema kuwa alikuwa na mpenzi wake ambaye ni mwarabu na alipokuwa kule alikaa mwenyewe ila akupokonywa passport na wala akuzidisha muda wa kukaa nchini humo.

Rachel amesema hata taarifa za yeye kuwa kwenye hali mbaya akitumia madawa ya kulevya hazina ukweli, hivyo watu wasiamini maneno wanayoyasikia kwa watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *