Mwanamuziki wa Marekani, R Kelly aonyesha masikitiko yake dhidi ya shutuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili, katika kipindi kimoja cha asubuhi cha televisheni.
Ikiwa ni mara ya kwanza mwanamuziki huyo kuhojiwa tangu akamatwe na polisi mwezi uliopita alisema,”Sijafanya vitu hivyo, huyo sio mimi ” na kusisitiza kuwa anapambania maisha yake.
Mwendesha mashitaka wa Chicago alimfungulia Kelly mashtaka 10 yanayohusiana na makosa ya unyanyasaji wa kingono, huku yakihusisha waathirika wanne ambao watatu kati hao walifanyiwa unyanyasaji wakiwa na umri chini ya miaka 18 .
R kelly alisisitiza kutokuwa na hatia kwa mashtaka yote yanayomkabili na sasa yuko nje ya gereza kwa dhamana.
Kama atapatikana na hatia, mwanamuziki huyo atatakiwa kufungwa kati ya miaka mitatu hadi sita kwa kila kosa.
Mwaka 2002, Kelly alikabibiliwa na mashitaka 21 ya kutengeneza filamu ya ngono na msichana ambaye alidaiwa kuwa chini ya umri wa miaka 18.
Na hatimaye jaji alihitimisha kesi hiyo kwa kusema kuwa hawawezi kuthibitisha umri wa binti yule kupitia mkanda wa video na hivyo kumpelekea Kelly kupatikana hana hatia kwa mashitaka yote 21.
Mwanamuziki huyo akizungumza na mwandishi Gayle King, Kelly alisema kesi ile ya awali imetumika dhidi ya mashitaka haya mapya ili kuaminika kuwa ana makosa kweli.
Mwanamuziki huyo alikana kuhusika na shutuma ambazo zilitolewa hivi karibuni dhidi ya makala yake mpya ya ‘Surviving R Kelly’, ambapo alikuwa amewakamata wanawake bila idhini yao na kuchukua simu zao, kuwakataza kula na kuwazuia kuwasiliana na familia zao.