Mwanamuziki wa R&B, R Kelly amekana madai ya kuwanyanyasa wanawake kingono.

Wakili wa mwanamuziki huyo amesema kuwa atatumia kila njia kuhakikisha kuwa wale wanaomtuhumu anawakabili kisheria ili kusafisha jina lake.

Ripoti ya BUzzFeed imemtuhumu mwanamuziki huyo kwa kuwabadili kimawazo wanawake walio karibu naye kwa lengo la kuimarisha usanii wao wa muziki.

Kelly tayari amewahi kukabiliwa na tuhuma za dhulma za kingono lakini hakupatikana na hatia.

Ripoti hiyo iliowanukuu wazazi watatu inasema kuwa hawajawasiliana na wanao kwa miezi kadhaa ,na kwamba wanawake hao wote wakiwa na umri wa zaidi ya miaka 18 walikuwa wakidhibitiwa na msanii huyo.

Udhibiti huo unashirikisha chakula wanachokula na nguo wanazovaa ,wakati gani wa kuoga na kulala mbali na kufanya tendo la ngono yote hayo yakirekodiwa na msanii huyo.

Wanachama watatu walio karibu na mwanamuziki huyo pia walihojiwa na kusema kuwa wanawake sita wanaishi katika nyumba zinazosimamiwa na msanii huyo.

Iwapo watavunja sheria, wanasema wanawake hao huadhibiwa kwa kupigwa mbali na kutukanwa na msanii huyo kulingana na ripoti hiyo.

Baadhi ya wazazi wao wameripoti wasiwasi kwa polisi, lakini wanawake hao wanasema kuwa wamekubali kuishi katika nyumba hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *