Maandalizi ya mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2021 yako katika hatua za mwisho ambapo mrembo Queen Mugesi ataiwakilisha Tanzania katika kilele kitakachofanyika Desemba 17, 2021 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Queen ambaye aliwashinda warembo zaidi ya 2,600 wa Tanzania walioomba kuiwakilisha nchi kwa njia ya mtandao, alichaguliwa katika mchakato ulioendeshwa na wataalamu wa mambo ya urembo kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Makamu wa Rais wa mashindano hayo, Jolly Mutesi alisema tayari nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo zimeshatuma wawakilishi wake na washiriki hao kwa sasa wapo katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.

Amesema nchi zilizokwisha tangaza wawakilishi wake ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, South Sudan na Somalia huku zingine ni Reunion, Ethiopia, Malawi, Burundi na Mauritius.

Amesema, mashindano ya Miss East Africa ambayo yaliasisiwa na Mtanzania Rena Callist mwaka 1996, yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa mambo ya urembo na yanatarajiwa kuangaliwa na zaidi ya watu milioni 200 moja kwa moja LIVE kupitia katika TV na wengine wengi zaidi wataangalia kupitia mtandao duniani kote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *