Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Queen Darleen ametoa ushauri mzito kwa Harmonize kuhusu maisha yake ya kimuziki na mahusiano.

Muimbaji huyo amemshari Harmonize kutokata tamaa na muziki wake ingawa watu wa kumkatisha tamaa wapo, huku akimsisitiza kuwa kuepeka kuwa katika mahusiano na wanawake wengi.

“Apunguze uhuni, atulie, mtoto wa watu masikini ya Mungu, Mzungu (Sarah) anampenda, yeye muhuni. Mdogo wangu maisha ya uhuni siyo mazuri, unakuwa kama mfalme Sulemani, ache hizo,”.

Harmonize na Queen Darleen wameshakutana katika ngoma inayokwenda kwa jina la Zilipendwa ambayo ilikutanisha wasanii kama Diamond, Lava Lava, Rayvanny, Rich Mavoko na Mbosso.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *