Waziri wa fedha wa Qatar, Ali al-Emadi amesema kuwa nchi hiyo itatumia karibu dola milioni 500 kwa wiki kwa miradi mikubwa wakati inajiandaa kwa Kombe la Dunia la mwaka 2022.

Ali al-Emadi amesema kuwa matumizi hayo ya fedha kuendelea kwa kipindi cha miaka mitatu au minne inayokuja kwa kujenga viwanja vipya, barabara, reli na hospitali.

Lakini bwana Emadi amekana kuwa mipango hiyo huenda ikisababisha kinyanganyiro hicho cha mwaka 2022 kuwa ghali zaidi duniani.

Kombe la dunia la mwaka 2014 lililoandaliwa nchini Brazil, liliripotiwa kugharimu dola bilioni 11 kuandaliwa, huku nayo Urusi ikiongeza bajeti ya kuandaa kombe la mwaka 2018 hadi dola bilioni 10.7.

Wanakandarasi nchini Qatar, wamewaleta maelfu ya wafanyakazi wahamiajia hasa kutoka mataifa ya kusini mwa Asia, ambao wapiganiaji wa haki za binadamu wanasema kuwa wanalazimishwa kufanya kazi katika mazingira mabaya.

Serikaloi ya Qatar imekana haya na mwezi Disemba ilifanya mabadiliko yenye lengo la kuboresha haki za wafanyakazi wahamiaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *