Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, aliyewahi kutamba miaka ya nyuma Q-Jay ameibuka na kukana vikali taarifa zilizoenea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amerukwa na akili.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja siku kadhaa baada ya kusambaa taairifa kuwa mwanamuziki huyo amechanganyikiwa kabisa mpaka kufikia kuwa chizi wa kuokota makopo.

Taarifa hizo zilisambazwa na msanii mwenzake anayejuliaka kama Makamua ambaye aliwaomba Watanzania wamchangie Q- Jay kwa madai ameathirika na madawa ya kulevya kiasi cha kuanza kuokota makopo.

Baada ya kusambaa kwa taarifa hizo Q Jay ameibuka na kuzikana vikali habari hizo zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii.

Pia Q- Jay amelaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kudai taarifa hiyo ilikuzwa kutokana na watu kutumia mitandao ya kijamii vibaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *