Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Q Chilla ameachia rasmi orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya itkayotoka mapema mwaka huu.

Q Chilla ameweka kava linaloonyesha orodha hiyo ya nyimbo zinazopatikana kwenye album yake aliyoiita ‘The Last Meal’ TLM huku ikiwa inaonekana imebeba nyimbo 10 na ikiwa na kolabo 4 tu na kuandika ‘Being is becoming watu wangu’.

Wasanii aliowashirikisha ni pamoja na mkongwe mwenzake katika muziki wa Bongo Fleva, Profesa Jay, Dogo Janja, Kusah na Tamimu ambao wote amewashirikisha kwenye albam hiyo.

Q Chillah alitangaza mapema mwaka huu kuwa anatarajia kuachia albam kwani kila kitu tayari kimekamilika kilichobaki ni kuiachia tu kwa mashabiki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *