Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa.
Ushindi huo ulitarajiwa katika upigaji kura uliomalizika siku ya jumapili.Hata kabla ya kura zote kuhesabiwa tayatri alikuwa amejizolea asilimia 76 kwa mjibu wa tume ya uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi amsema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake.
Putin ameongeza kuwa hii ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano.
Ushindi huu mkubwa ambao ulitarajiwa,umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012.Ambapo m,pinzani wa karibu wa Putin milionea Pavel Grudinin,yeye alipata asimilia 12.