Rais wa Urusi, Vladimir Putin amesema kuwa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameridhia kuungana na mataifa yenye nguvu.

Putin amesema yuko tayari kurudisha mahusiano yao yaliyokuwa yanaenda mrama kutokana na mzozo wa Ukraine na Syria ingawa tarehe ya kukutana kwao haijatajwa bado.

kiongozi huyo wa Urusi pia amesema kuwa kulikuwa na tofauti kubwa kati ya sera na kampeni za kisiasa za Marekani.

Rais huyo mteule wa Marekani anaendelea kukutana wanachama muhimu wa bunge na mojawapo ya watu anaotazamia ni Jenerali James Mattis anayejulikana kwa kikosi chake kama mbwa mwenye hasira ambaye ni mgombea anayeongoza katika kinyanganyiro cha kuwa waziri wa ulinzi wa marekani.

Kumekuwa na tetesi kuwa trump atamteua aliyekuwa mgombea wa Urais Mitty Romney katika ngazi ya juu ya uongozi, aliyewahi kusema kuwa Trump ni laghai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *