Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemlalamikia Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad kufungia akaunti zote za chama hicho za wilaya.
Profesa Lipumba amesema kutokana na uamuzi huo ruzuku ya chama kutoka serikalini wameikosa.
Mwanasiasa huyo amesema CUF ipo katika mtihani kwa sasa, hivyo uwapo wa Maalim katika kikao hicho ungesaidia kuiimarisha.
Amesema kuwa Maalim Seif alitakiwa kuhudhuria kikao hicho na alipewa taarifa lakini hakuweza kufika, hali iliyosababisha majukumu yake kusimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Tanzania Bara), Magdalena Sakaya kama katiba yao inavyoelekeza.
Akijibu tuhuma hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Mazrui amesema kuwa hatua ya kufunga akaunti za benki imelenga kulinda fedha ya chama ili zisitumiwe vibaya na upande wa Profesa Lipumba.