Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka amesema kuwa hatogombea tena nafasi ya ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

Profesa Tibaijuka amesema kuwa umri wake umekwenda na kizazi chao kimeshamaliza kazi na sasa anawaachia vijana waendeleze kurudumu la maendeleo kwa taifa la Tanzania.

Tibaijuka alitangaza uamuzi huo walipokuwa wakizungumzia miaka miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tangu aingie madarakani ambaye alikuwa kwenye ziara mkoani Kagera.

Tibaijuka amekuwa mbunge wa jimbo hilo tangu mwaka 2010, na alishawahi kukumbwa na kashfa kubwa ya pesa za Escrow na kumfanya aondolewe katika nafasi ya Uwaziri katika serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Kikwete.

Profesa Tibaijuka pia alishawahi kufanya kazi katika shirika la makazi la Umoja wa Mataifa (UN habitat) ambapo kituo chake cha kazi kilikuwa nchini Kenya.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *