Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Iblahim Lipumba amesema kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Hammad endapo ataomba radhi katika atasamehewa na kukabidhiwa ofisi yake iliyopo Buguruni jijini Dar.

Lipumba ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kamati ya maadili na nidhamu ambayo ameeleza kuwa itakuwa na jukumu la kumhoji katibu mkuu huyo.

Ameeleza kuwa miongoni mwa mambo atakayohojiwa ni kuhusiana na suala la kukihujumu na kukidharirisha chama hicho pamoja na kujihusisha na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 Hivyo ameeleza kuwa Kama endapo kiongozi huyo atayakiri makosa yake hakutakuwa na sababu ya kuendelea kulumbana kwani muda huu niwakukijenga na ofisi yake ipo wazi atakabidhiwa akikiri makosa yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *