Mwenyekiti anayet wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amemshutumu Maalim Seif Sharif Hamad kuwa kwa anataka kukiua chama hicho.

Lipumba alitoa tuhuma hizo jana, wakati wa kongamano la Jumuiya ya Vijana wa CUF (Juvicuf), lililofanyika kwenye ofisi za chama hicho Buguruni.

Akihutubia kongamano hilo alimtuhumu Maalim Seif kwa madai ya kubadili utaratibu wa vikao vya ushauri kwa kuzungumza na mkurugenzi mmoja mmoja badala ya kuwaweka pamoja.

Alisema kitendo hicho ni cha kumdhalilisha Naibu Katibu mkuu wa chama hicho Bara, Magdalena Sakaya.

Alisema huu ni wakati wa kukijenga chama na hakuna mwanasiasa bara aliyefanya kazi kubwa kuwatetea Wazanzibari kama yeye (Lipumba).

Hata hivyo, Lipumba alisema amemsamehe Maalim Seif na yupo tayari kukaa naye meza moja ili kukijenga chama hicho ikiwamo kujenga uchumi utakaoleta manufaa kwa wananchi.

Pia, Lipumba alikishutumu Chama cha Chadema kwamba kinamhadaa Maalim Seif na kinaweza ‘kumuuza’ kama kilivyofanya kwa Dk Wilbrod Slaa na kwamba hakina demokrasia kama kinavyotamba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *