Nyota wa muziki nchini Marekani, David Bowie na Prince ni miongoni wasanii wa hivi karibuni waliorodheshwa na kampuni ya Forbes kuwa miongoni mwa watu maarufu waliofariki ambao wanapata mapato ya juu.
Mapato ya Prince kabla ya kutozwa kodi mnamo tarehe 1 mwezi Oktoba yalifikia dola milioni 25 kulingana na jarida la biashara la Business Magazine akiwa wa tano katika orodha hiyo.
Bowie, yuko katika nafasi 11 kwa makadirio ya mapato ya kiasi cha dola milioni 10.5.
Wote wawili hatahivyo wamepitwa na nyota wa muziki wa Pop marehemu Michael Jackson ,ambaye anaongoza orodha hiyo kwa mara nyengine akivunja rekodi ya makadirio ya mapato ya kiasi cha dola milioni 825.
Forbes inasema kuwa kitita hicho ni kikubwa kuwahi kupatwa na mtu maarufu kwa mwaka mmoja, kutokana na kuchapishwa kwa muziki wake uliouza kwa kitita cha dola milioni 750.
Jackson anamiliki asilimia 50 ya hisa katika kampuni ya muziki ya Sony ATV Music Publishing ,maarufu kwa nyimbo zake za Beatles ikiwa ni ushirikiano wa kibiashara ulioanza 1995.